Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzanian Training Centre for International Health, (TTCIH) anawatangazia umma nafasi za kujiunga na chuo kwa mwaka wa masomo 2023/2024. TTCIH ni Taasisi ya mafunzo ya Afya Ifakara iliyosajiliwa na NACTVET kwa namba HAS/003, Chuo kipo Ifakara mjini, Mkoani Morogoro. Chuo kina mazingira tulivu na mazuri kwa kujifunza ikiwa pamoja wakufunzi wabobezi katika masomo yote, Hospitali ya kujifunzia, maktaba bora na masomo kwa njia ya kielektroniki yaani eLearning