Udahili Mwaka wa Masomo 2022/23
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzanian Training Centre for International Health, (TTCIH) anawatangazia umma nafasi za kujiunga na chuo kwa mwaka wa masomo 2022/2023. TTCIH ni Taasisi ya mafunzo ya Afya Ifakara iliyosajiliwa na NACTVET kwa namba HAS/003, Chuo kipo Ifakara mjini, Mkoani Morogoro.
Chuo Kinatoa Kozi Zifuatazo
- Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) – Miaka Mitatu
- Stashahada ya Utabibu ya Mwaka Mmoja (Yaani Upgrading from Clinical Assistant to Clinical Officer).
Sifa za Mwombaji kwa Kozi zote
Sifa za Mwombaji kwa Kozi ya Stashahada ya Utabibu ya Miaka Mitatu awe
- Awe amehitimu kidato cha nne kwa ufualu wa angalau D ya Biology, Chemistry na Physics
Sifa za Mwombaji wa Stashahada ya Utabibu Mwaka Mmoja (Yaani Upgrading From Clinical Assistant to Clinical Officer )
- Awe amehitimu Astashahada ya Utabibu (Technician Certificate in Clinical Medicine).
Chuo kina mazingira tulivu na mazuri kwa kujifunza ikiwa pamoja wakufunzi wabobezi katika masomo yote, Hospitali ya kujifunzia, maktaba bora na masomo kwa njia ya kielektroniki yaani eLearning
Jinsi ya Kujaza Fomu za Maombi
Maombi yote ya kujiunga na Chuo yanatumwa kupitia tovuti ya NACTVET kwenye kiunganishi (QUICK LINK ) Kilichoandikwa “MAOMBI YA UDAHILI VYUO VYA AFYA“
KARIBU TTCIH IFAKARA KWA MAFUNZO YENYE KUJENGEA WAHITIMU UWEZO KUTOA TIBA KWA KUTUMIA TAFITI YAANI EVIDENCE BASED MEDICINE
Kwa msaada na maelekezo zaidi piga simu namba(+255) 0758943044 || 0787629707





