Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mafunzo ya Afya ya Ifakara (Tanzanian Training Centre for International Health ) – TTCIH iliyopo mjini Ifakara Mkoani Morogoro anawatangazia umma kwamba sasa DIRISHA LA UDAHILI lipo wazi kwa  kozi zifuatazo  kwa mwaka wa masomo 2023/2024.

Chuo Kinatoa Kozi Zifuatazo;

Sifa za muombaji kwa kozi ya stashahada  ya Utabibu (miaka mitatu)awe:

  • Amehitimu kidato cha nne kwa ufualu wa angalau D ya Biology, Chemistry na Physics

Sifa za muombaji kwa kozi ya stashahada  ya Optometria (Miaka mitatu) awe na:

  • Amehitimu kidato cha nne kwa ufualu wa angalau D ya Biology, Chemistry, Basic Mathematics, English  na Physics/Engineering Sciences

Sifa za muombaji kwa kozi ya stashahada  ya Ufamasia (miaka mitatu) awe na:

  • Amehitimu kidato cha nne kwa ufaulu wa angalau D ya Biology na Chemistry

Sifa za muombaji kwa kozi ya stashahada  ya Health Information Sciences  (Miaka mitatu) awe na:

  • Amehitimu kidato cha nne kwa ufualu wa angalau D ya Biology, Basic Mathematics na English Language
TTCIH ni Taasisi ya Serikali iliyosajiliwa na NACTEVET kwa namba HAS/003 inayoendeshwa chini ya Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoka inchini Uswiss. Taasisi ina mazingira tulivu na mazuri kwa kujifunza ikiwa pamoja Wakufunzi waliobobea katika fani za Afya na tafiti, Hospitali ya kujifunzia kwa vitendo, Internet ya uhakika, na kutoa mafunzo kupitia Mfumo wa Mafunzo kwa njia ya Masafa – (National eLearning Platform for Health – www.elearning.moh.go.tz) ambao unasimamiwa na Wizara ya Afya.

Tip: Resize the browser window to see how the value "justify" works.

Kwa msaada na maelekezo zaidi na pamoja na kujaza fomu za maombi  piga simu namba zifuatazo +255718 552164, +255758 943 044, +255787629707 au tutumie barua pepe info@ttcih.ac.tz

Previous Post
Newer Post